Timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu ya wasichana wenye umri wa chini ya miaka 20 ya Nigeria ‘Falconets’ inatarajiwa kutua nchini usiku wa kumkia Ijumaa Septemba 29, kuvaana na Tanzanite kwenye mchezo wa marudiano kuwania kucheza fainali za Kombe la Dunia
Mchezo huo wa marudiano utafanyika Jumapili Oktoba mosi, mwaka huu kwenye Uwanja wa Azam ulioko Chamazi, Dar es Salaam kuanzia saa 10.00 jioni.
Tanzania ina matumaini ya kufanya vema kwenye mchezo huo wa marudio licha ya kupoteza kwa mabao 3-0 katika mchezo wa kwanza uliofanyika Uwanja wa Samwel Oigemudia ulioko Jimbo la Benin, Nigeria.
Timu hiyo ya wasichana yenye wachezaji 18, watatua Dar es Salaam saa 9.40 usiku na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, limewapangia kuishi katika Hoteli ya Urban Rose iliyoko katikati ya jiji la Dar es Salaam katika kipindi cha siku tatu watakazokuwa hapa jijini.
Aidha kikosi hicho kutokea Nigeria kinatarajiwa kuwa cha watu 31 huku miongoni mwake wakiwa wako maofisa 13. Fainali za Kombe la Dunia zitafanyika Ufaransa hapo mwakani.

Related posts
Nigeria kutua Dar kupambana na Tanzanite
Reviewed by Informalblogsport
on
13:46
Rating: 5
No comments: