MSANII kutoka nchini Nigeria ambaye pia ni ‘hitmaker’ wa nyimbo za If na Fall, Davido, amesema hatajibu tena meseji za DM baada ya kuzinguliwa na mtoto mmoja mrembo aliyejulikana kama Sheila.
Davido alikerwa na tukio hilo kwa kuposti video clip akisema hatajibu tena DM kwa kuwa Sheila alijitapa kwamba msanii huyo alimcheki DM na kuchati naye. Kitendo hicho kimemfanya Davido akasirike huku akidai kuwa binti huyo ndiye aliyeanza kumshobokea.
Sheila alipost picha yenye chati yake na Davido akiandika:
“No better feeling than waking up to Davido’s text… We all have tastes and differences… I like my male friends Black and Moneyed!” Alisema hakuna kitu cha furaha kama kuamka na kukutana na meseji ya Davido, tuna machaguo tofauti, napenda jamaa zangu wa kiume wa Afrika na wenye mkwanja.
Baada ya hapo Davido akaamua kujibutua insta na kuweka chati yao halisi na kumchana Sheila alivyomsingizia kwamba alianza kuzama DM na kusema kuwa hatajibu tena DM za watu kwenye account zake
No comments: