Patashika ya Ligi Kuu ya soka ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) kuwaka moto kama kawaida wikiendi hii ndani ya Azam TV, Burudani kwa wote. ...! Ijumaa hii, Oktoba 13, Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza utakuwa katika wakati mgumu pale wenyeji Mbao FC watakapokipiga na Mbeya City FC, utashuhudia kipute hiki mbashara kupitia Azam Sports 2, kuanzia saa 10:00 jioni.
Jumamosi sasa mji wa Kagera utasimama kwa mda ukipisha mtanange maridhawa baina ya Kagera Sugar dhidi ya Mabingwa watetezi Yanga SC mechi hii itakuwa mbashara Azam Sports 2 kuanzia saa 10:00 jioni, mda huo huo kupitia Azam TWO utashuhudia mtanange mkali kati ya Mwadui FC dhidi ya Mabingwa Afrika Mashariki na Kati Azam FC.
Jumapili sasa Oktoba 15, nyasi za Uwanja wa Uhuru, Jijini Dar es Salaam zitahimili kishindo cha mchezo wa timu zilizofungana pointi katika usukani wa Ligi ya VPL Simba SC 'Wekundu wa Msimbazi' na wakata miwa wa manungu Mtibwa Sugar utashuhudia mchezo huu Live Azam Sports 2
No comments: