Sheria inayoiga marufuku vazi la kiislamu katika sehemu za umma imeanza kutekelezwa nchini Austria.
Serikali inasema kuwa sheria hiyo inayosema kwa uso lazima uonekane ni ya kulinda tamaduni za Austria.
Inakuja kabla ya uchaguzi mkuu baadaye mwezi huu ambapo chama cha mrengo wa kulia cha Freedom kinatarajiwa kupata mafanikio.
Makundi ya waislamu yamekosoa sheria hiyo yakisema kuwa ni watu wachache waislamu nchini Austria ambao huvaa Niqab
Sheria inapiga marufuku mavazi ya kiislamu kama burka na Niqab.
Takriban wanawake 150 huvaa burka nchini Austria lakini maafisa wa kitalii wanasema kuwa hatua hizo pia zitawazuia wageni kutoka nchi za Ghuba.
Ufaransa na Ubelgiji zilipiga marufuku vazi la burk mwaka 2011 na hatua kama hiyo kwa sasa inazungumziwa katika bunge la Uholanzi.
Chansela wa Ujerumani Angela Merkel amesema kuwa vazi la kufunika uso wote litapigwa marufuku nchini Ujerumani
No comments: