Muigizaji wa Filamu Bongo, Faiza Ally amefunguka kuupa zaidi muziki wa Alikiba kuliko ule wa Diamond.
Faiza amesema hayo katika mahojihano na TBC Fm kwa kueleza kuwa Diamond ni mburudishaji wa jumla aliyeleta mapinduzi ya kimuziki lakini Alikiba muziki wake ni bora zaidi.
“Kwanza kati ya muziki wa Diamond na Alikiba, naupenda sana muziki wa Kiba, muziki wake ni mzuri kuliko wa Diamond,” amesema Faiza na kuendelea.
“Diamond ni ile full Entertainment ukimwalia tu unatabasamu lakini Kiba ana muziki mzuri. Nikizungumzia mtu aliyeutoa muziki akaupa heshima mpaka akampa changamoto Kiba na yeye akasimama mpaka tukaanza kumuona kwenye hali ya tofauti ni Diamond,” amesema.
Ikumbukwe kuwa September 3 mwaka huu Faiza aliandika ujumbe katika mtandao wa Instagram na kueleza kuwa kumpenda Diamond ni jambo la lazima na sio ombi kutokana na mengi mazuri aliyofayanya katika muziki wa Bongo Flava.
No comments: