Kauli ya Zitto baada ya Gazeti la Raia mwema kufungiwa

Muda mchache baada ya Serikali kuchukua hatua dhidi ya gazeti la RAIA MWEMA. kwa lifungia ndani ya muda wa siku 90 kwa kile ilichodai kuwa limetunga nukuu za uongo dhidi ya Rais, Mbunge wa Kigoma mjini Zitto Kabwe ameandika ujumbe huu kupitia ukurasa wake wa Facebook.
"Serikali ya CCM ya Awamu ya 5 inaongoza kufungia magazeti kuliko Serikali zote zilizopita. Sababu za Kufungia gazeti la RaiaMwema hazina msingi wowote na ni aibu kubwa. 

Ukosoaji unaofanywa na RaiaMwema ni ukosoaji wenye staha unaopaswa kulindwa kwenye jamii yeyote yenye kuheshimu demokrasia.

Kama hutaki kukosolewa huna sifa ya kuwa Kiongozi wa Umma, tena kwenye Nchi ya wastaarabu Kama 




No comments: