Dangote Amtahadhariha Rais Magufuli Kuhusu Sera Mpya za Uwekezaji



ajiri namba moja barani Afrika Aliko Dangote ambaye pia ni mwekezaji mkubwa hapa nchini amemtahadhariha Rais John Pombe Magufuli kuwa sera zake mpya zinawaogopesha wawekezaji.
Dangote ambaye amewekeza dola za kimarekani 650 kwenye uzalishaji wa saruji, amesema ni wakati umefika kwa raisi Magufuli kuzipitia upya sera zake ama akubali kuingia katika hatari ya kuwapoteza wawekezaji wote nchini .
Dangote ameyasema hayo katika mkutano wa FT Afrika unaofanyika London Uingereza na kuhudhuriwa na watu mashuhuri kutoka maeneo mbalimbali duniani.
Mwekezaji huyo ameeleza kuwa Uhusiano wake na Rais Magufuli ni mzuri lakini akashauri Rais azipitie upya sera zake kama anataka kuwavutia waekezaji wengi zaidi.
“Uhusiano wangu na Rais Magufuli uko sawa lakini Tanzania lazima itazame upya sera zake kama inataka kuvutia wawekezaji,” alisema Dangote.
Dangote pamoja na watu wengine mashuhuri wakiwemo viongozi wa maeneo mbalimbali duniani wamehudhuria mkutano huo wa FT Africa wenye lengo la kuangazia changamoto zinazolikumba bara la Afrika na namna ya kuzitatua unaofanyika kila mwaka na mwaka huu umefanyika huko London, Uingereza kuanzia Oktoba 8 hadi Oktoba 9.
Kauli mbiu ya mkutano huo ni ‘what is working in Africa’ ikiwa na maana ya ‘nini kinachofanya kazi katika Afrika’ ikiwa na dhumuni la kuangazia ni kwa namna gani bara hilo linaweza kunufaika kutokana na fursa, rasilimali na utajiri uliopo humo.

No comments: