Baada ya kukamatwa na kuachiwa kwa kosa la ubakaji rapa Nelly amesema hajafanya kosa hilo na kwamba aliyefungua mashtaka amesema uongo.
October 7 2017 rapa Nelly alikamatwa na kuhojiwa na polisi kwa muda mfupi kabla ya kuachiwa bila dhamana ikiwa ni saa chache toka mwanamke mmoja kutoka mjini Washington kusema amebakwa na staa huyu.
Dada huyo anasema alibakwa na Nelly kwenye basi lake la Tour baada ya show yake huko White River Amphitheater, tuhuma ambazo wakili wa Nelly amesema sio za kweli.
Nelly,42, yupo kwenye tour sehemu tofauti Marekani na mpaka sasa hakuna taarifa zozote kuhusu kesi hii kudhuru mauzo ya ticket z show yake,
No comments: