Chanzo, Athari , Kinga na Tiba ya Ugonjwa wa Manjano

Image result for picha za ugonjwa wa manjano
Ugonjwa wa Manjano ambao hufahamika  kitaalamu kama HEPATITIS B ni  hatari  sana  na umesababisha vifo  vya mamilioni ya watu duniani kote. Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Afya Duniani  ( W.H.O ) kuna zaidi ya wau Milioni 350 duniani ambao wameathiriwa na ugonjwa huu hatari  kabisa na zaidi ya watu 620,000 hufa kila mwaka kwa ugonjwa wa Manjano.

CHANZO   CHA  UGONJWA  WA  MANJANO
Ugonjwa  wa  Manjano  husababishwa  na  virusi  viitwavyo  “ Hepatitis  B “ (  HBV )  ambavyo  hushambulia    zaidi ini  la  mwanadamu.   Virusi  hivi  visipo  tibiwa  mapema  hutengeneza  uvimbe  katika  ini  na  kusababisha  asratani  ya  ini  ambayo  hupelekea  kifo.

MAMBO  YASABABISHAYO  MAAMBUKIZI  YA  UGONJWA  WA  MANJANO.
Ugonjwa    wa  Manjano  huambukizwa  kwa  njia  zifuatazo  :
  • Kujamiiana  bila  kutumia  kinga.
  • Kunyonyana  ndimi
  • Kuchangia  damu  isiyo  salama
  • Mama mjamzito mwenye ugonjwa huu anaweza kumuambukiza mtoto wake wakati  wa kujifungua.
  • Kuchangia  vitu  vyenye  ncha  kali  kama  vile  wembe  na  sindano.

DALILI  ZA  UGONJWA  WA  MANJANO
Dalili  za  ugonjwa wa  manjano  huchukua  muda  mrefu  kuonekana  tangu  maambukizi  yatokee, na  zinapo  anza  kuonekana  wazi  wazi, mgonjwa  anakuwa  amesha  athirika  kwa  kiwango kikubwa  sana.  Dalili  za  ugonjwa   huu  ni  kama  ifuatavyo :
  • Uchovu  wa  mwili
  • Kichefuchefu
  • Mwili  kuwa  dhaifu
  • Homa  kali
  • Kupoteza  hamu  ya  kula
  • Kupungua  uzito
  • Kupatwa  na  maumivu  makali  ya  tumbo upande  wa  ini.
  • Kukojoa  mkojo  wa  rangi  nyeusi
  • Macho  na  ngozi  kuwa  vya  njano.

KINGA   YA  UGONJWA  WA  MANJANO
  • Kupatiwa  chanjo  ya  kujikinga  na  maambukizi  ya  ugonjwa  huu.
  • Kutumia  kinga  wakati  wa  kujamiiana
  • Kuacha   kuchangia  vitu  vyenye  ncha  kali  kama  sindano, wembe  n.k
  • Kutochangia  mswaki
  • Kuwa  na  mpenzi  mmoja  mwaminifu
  • Kuto ongezewa damu  ambayo  haijapimwa  na  kuthibitika  kuwa  salama.

TIBA   YA  UGONJWA  WA  MANJANO
Ugonjwa  wa  manjano  hauna  tiba  isipokuwa  mgonjwa   akiwahi  hospitali  atapatiwa  dawa za kupambana  na  virusi  kuvipunguza  nguvu  za  kupambana  na  ini., kupandikizwa  ini  ambapo ini lililoathirika  huondolewa  na  kuwekwa  jingine  japo  ni  vigumu  kupata  ini  salama.

Ukisha  gundua  kuwa  umeambukizwa  ugonjwa  huu  unashauriwa   kuacha  kutumia  pombe, dawa za  kulevya  na  vitu  vingine  vinavyo  athiri  utendaji  kazi  wa  ini.

No comments: