Tambua kile unachokitaka, hapa inabidi uelewe nini unachokitaka. Kama unataka kuongozeza uhuru wa kifedha hilo pia unatakiwa kulijua. Unatakiwa kukijua kile unachokitaka kwa uwazi sana.
Andika malengo yako chini, malengo yasiyondikwa ni kama moshi wa sigara wakati wowote ni rahisi kupotea. Malengo ambayo yameandikwa yanakuwa ya muhimu kwenye akili na utendaji unakuwa rahisi pia.
Weka tarehe ya mwisho kufikia malengo yako, kama ni malengo makubwa weka tarehe ndogo ndogo za kukamilisha malengo yako. Unapoweka tarehe hiyo akili yako inakuwa inafanya kazi kwa nguvu sana kuhakikisha malengo yanatimia.
Andika orodha ya mambo yatakayokusaidia kutimiza malengo yako, hapa andika watu, maarifa unayohitaji na hata vizuizi ambavyo vinaweza kujitokeza na jinsi ya kuviepuka ili ufanikiwe.
Weka orodha ya vipaumbele vyako, vipaumbele vinakusaidia kujua kipi cha muhimu na kipi ambacho sio cha muhimu katika kutimiza ndoto zako. Hutaleta mchezo ukishawea vipaumbele vya malengo yako.
Chukua hatua haraka sana, usichelewe katika kuchukua hatua, kuahirisha mambo ni adui mkubwa sana wa ndoto zako na unapoahirisha mambo kila wakati ni sawa na kujiibiwa mwenyewe kwenye maisha yako.
Fanya kila siku kitu cha kukusogeza kwenye malengo yako, hii ni hatua muhimu sana ambayo inakuhakikishia mafanikio yako. Fanya kitu fulani katika siku saba za wiki, fanya kitu kwa mwaka mzima, utafanikiwa.
No comments: