Kashifa za Haji Manara kwa Yanga



Kama kawaida yake, Mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano cha klabu ya Simba SC, Haji Manara amekua mmoja wa watu ambao wanaendelea kulifanya soka la kibongo kupendwa zaidi hasa akeendelea kuunogesha ule usemi uitwao watani wajadi.
Katika kuhakikisha anatimiza jukumu lake Mkuu huyo leo ametupia utani wake upande wa pili baada ya kumalizika kwa mtanange wa kirafiki kati ya klabu hiyo ya Yanga yenye maskani yake mitaa ya Twiga na Jangwani.
Manara kupitia Akaunti yake ya Instagram ameposti ujumbe unaosomeka hivi"Eti lile kunde lililopigwa kule chamazi limeishaje? Mnijalie matokeo na kama jamaa wamepata mpunga wa kwenda kanda ya ziwa."

Yanga ambao ndio wapinzani wakubwa wa Simba leo jioni wametelemka dimbani kumenyana na klabu ya KMC( Kinondoni Manicipal Council) katika mchezo wa kirafiki mchezo ambao umemalizika kwa timu zote kutoliona lango la mwezake.

No comments: