Michuano ya Klabu bingwa barani Ulaya inatarajia kuanza kutimua vumbi hii leo usiku kwa michezo kadhaa kupigwa katika hatua ya makundi.
Vinara wa Ligi Kuu ya Uingereza klabu ya Manchester City hii leo watakuwa wenyeji kuwakaribisha, Shakhtar Donetsk katika mchezo ambao utavuta mashabiki wengi hapo Uingereza kutokana na ubora waliyonao kwa sasa vijana wa Mhispania, Pep Guardiola, ukiwa ni mchezo wa kundi F.
Katika mchezo mwingine wa kundi hilo F, timu ya Napoli itakuwa mwenyeji katika dimba la Stadio San Paolo, Naples ambapo itawakaribisha Feyenoord.
Wakati huo vijana wa Jurgen Klopp klabu ya Liverpool hii leo wapo ugenini nchini Urusi kuwavaa Spartak Moskva mchezo utakao pigwa katika dimba la Otikrytie Arena, Moscow.
Michezo ya leo ya makundi ya Klabu bingwa barani Ulaya
Kundi E – Sevila inacheza na Maribor, Spartak Moscow dhidi ya Liverpool,
Kundi F – Manchester city inacheza na Shakhtar Donetsk, Napoli inacheza na Feyenoord.
Kundi G- Besiktas inacheza na Rasen Ballsport , Monaco dhidi ya FC Porto.
Kundi H – Apoel Nicosia dhidi ya Tottenham na Borussia Dortmund inachuana na Real Madrid.
Kesho Jumatano Septemba 27
Kundi A – FC Basel itacheza na Benfica, CSKA Moscow na Manchester United.
Kundi- B Anderlecht dhidi ya Celtic, PSG itakwaruzana na Bayern Munich.
Kundi C- Qarabag dhidi ya As Roma, Atletico Madrid wanakutana na Chelsea,
Kundi – D Juventus itacheza na Olympiacos huku Sporting ikichuana na Barcelona
Ratiba ya michuano ya Klabu bingwa barani Ulaya .
No comments: