Wapiganaji waendeleza mashambulizi Mali


Vikosi vya Umoja wa Mataifa, MaliHaki miliki ya pichaMINUSMA/MARCO DORMINO
Image captionVikosi vya Umoja wa Mataifa, Mali
Umoja wa Mataifa umesema mashambulizi yanayofanywa na wanamgambo wa kiislamu dhidi ya majeshi ya serikali ya Mali, Walinda Amani wa Umoja wa Mataifa na Vikosi vya jeshi la Ufaransa, yameongezeka mfululizo.
Kumefanyika mashambulizi 75 kati ya mwezi Juni na Septemba, mara mbili zaidi ya yale yaliyotokea miezi minne awali.
Majeshi ya Mali yamekuwa yakishambuliwa vibaya. Nalo Jeshi la kulinda amani la Umoja wa Mataifa nchini humo limeelezea eneo hilo kama ni la hatari duniani.
Nchi hiyo imekuwa haina udhabiti tangu waasi wa Tuareg wanaotaka kujitenga na wapiganaji wenye itikadi kali walipodhibiti eneo la kaskazini miaka mitano iliyopita.

No comments: