Mlinzi wa zamani wa klabu ya Manchester United na timu ya taifa ya England Rio Ferdinand amesema kujiunga kwake katika mchezo wa ndondi ni kwa sababu anataka kupunguza hasira na kumfanya asahau kipindi kigumu alichopitia.
Mke wake Rebecca alifariki akiwa na miaka 34 hii ni 2015 na Ferdinand akastaafu soka papo hapo.'Hii ni namna nyingine ya kupunguza hasira zangu, mawazo na kujiweka sawa zaidi,'' alisema Ferdinand mwenye watoto watatu.
Ferdinand anayefundiwa na kocha Richie Woodhall, amesema ananuia kupata ubingwa hivi karibuni.
Ferdinand ambaye ameshinda vikombe sita vya ligi kuu na kimoja cha ligi ya mabingwa Ulaya akiwa na Man U, huenda akafuata nyayo za kiungo wa zamani wa Birmingham City Curtis Woodhouse na mshambuliaji wa zamani wa Crystal Palace Leon McKenzie, ambao baada ya kuachana na soka waliingia katika ndondi za kulipwa.
No comments: