Viongozi wa Cataloni washutumiwa


HispaniaHaki miliki ya pichaAFP
Image captionMfalme wa Hispania Felipe akihutubia kwa njia ya runinga
Mfalme Felipe wa Hispania amezishutumu mamlaka za Kikatalani kwa kutokuwa na staha kwa kufanya kitendo cha kidhalimu na kukiita kisichofaa kwa kuruhusu kura ya maoni iliyopigwa siku ya Jumapili juu ya kudai uhuru.
Katika hotuba isiyo ya kawaida ambayo ni nadra kuhutubia taifa kwa njia ya runinga, Mfalme huyo ameiita kura hiyo ya maoni kuwa isiyo halali na ni kitendo cha kutoheshimu sheria , na kwa kitendo hicho ametabiri kuwa kunaweza kuwa hakuna amani na uhuru.
Ameshutumu medani za uongozi za watu wa Katalani kwa kutojali mambo, na kutoa wito wa kusimama imara katika ahadi ya kuwa imara kwa katiba.
Aliongoze kusema kuwa Hispania inapaswa kuwaunga mkono raia wake ambao wana mashaka na kile viongozi wao walichokuwa wakikifanya.
Maelfu ya watu wamekuwa wakiendelea na maandamano mjini Catalonia wakipingana na polisi kuhusiana na kura ya maoni iliyopigwa siku mbili zilizopita, katika kipindi hicho maelfu ya watu walijeruhiwa.

No comments: