Mwandishi akamatwa kwa ''habari ya nguo za ndani'' za Bi Mugabe


Bi Grace Mugabe adaiwa kuwagawanyia wafuasi wa Zanu PF ngu za ndaniHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionBi Grace Mugabe adaiwa kuwagawanyia wafuasi wa Zanu PF ngu za ndani
Maafisa wa polisi nchini Zimbabwe wanamzuilia mwandishi mmoja wa habari kuhusu taarifa yake iliodai kwamba mbunge mmoja wa chama tawala cha Zanu-PF aliwapatia wafuasi wa chama hicho nguo za ndani kwa niaba ya mke wa rais bi Grace Mugabe kulingana na mawakili wa ripota huyo.
Habari hiyo ilichapishwa katika jarida la Newsday, linalomilikiwa kibinafsi.
Polisi mashariki mwa mji wa Mutare walimkamata Kenneth Myangani siku ya Jumatatu jioni , mawakili wa haki za kibinaadamu walisema katika taarifa.
Mwandishi huyo kutoka Mutare huenda akakabiliwa na mashtaka ya ''uhalifu wa kumuharibia mtu jina'' baada ya kukamatwa kwa kuandika na kuchapish habari kuhusu ufadhili wa nguo za ndani zilizotumika na bi Grace Mugabe.
Kulingana na gazeti hilo, nguo hizo zilisambazwa na mbunge wa eneo hilo Esau Mupfumi ambaye alisema kuwa zilitolewa na bi Mugabe.
Wakili wa mwandishi huyo alisema kuwa haijulikani iwapo mlalamishi alikuwa mbunge huyo ama mke wa rais.
Hali mbaya ya kiuchumi nchini Zimbabwe inawalazimu watu wengi kununua nguo zilizotumika kulingana na chombo cha habari cha AFP.
Kinasema kuwa vitu hivyo ni kama vile nguo za ndani kutoka mataifa ya magharibi ambazo huingizwa nchini Mozambique kwa bei rahisi.
Mke wa rais bi Grace Mugabe alivutia vyombo vya habari mnamo mwezi Agosti wakati aliposhutumiwa kwa kumshambulia mwanamitindo katika hoteli moja ya Johannesburg ambapo watoto wake walikuwa wakiishi. Amekana kufanya makosa yoyote.

No comments: