Baadhi ya wachezaji wa klabu ya Barcelona yenye maskani yake katika jimbo la Catalonia nchini Hispania wameanza kurejea mazoezini baada ya kuziwakilisha timu zao za taifa katika kuwania tiketi ya kufuzu michuano ya kombe la dunia inayotarajiwa kufanyika nchini Urusi mwakani.
Tayari michezo ya kuwania kufuzu kwa michuano ya kombe la dunia inaelekea ukingoni na kwa sababu hiyo baadhi ya wachezaji wa kimataifa wa klabu ya Barça wameanza kurejea mazoezini chini ya meneja Ernesto Valverde tayari kujiandaa na Ligi Kuu nchini Hispania La Liga.
Wachezaji kama Ivan Rakitic, Jordi Alba na Sergio Busquets wamewasili katika timu hiyo na kuanza mazoezi leo asubuhi siku ya Jumatano na kuunga na Gerard Pique pamoja na Marc Andre Ter Stegen ambao wamewasili juzi.
Barca inakabiliwa na mchezo mgumu wa ugenini dhidi ya Atlético Madrid katika uwanja mpya wa Wanda Metropolitano huku Andrés Iniesta ambaye hivi karibuni ameingia mkataba mpya wa kudumu katika kikosi hiko cha Catalonia atakuwa katika eneo la Ciutat Esportiva la kujidai la Barcelona lenye hali joto ya 23ºC.
No comments: