JPM awaapisha mawaziri


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo amewaapisha Mawaziri 21 na Manaibu Waziri 21, aliowateua, baada ya kufanya mabadiliko ya Baraza hilo Oktoba 7, 2017.
Sherehe za kuapishwa kwao zimefanyika Ikulu jijini Dar es salaam, na kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali wa kitaifa, wakiwemo Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu Kasim Majaliwa, Spika wa Bunge Job Ndugai na Jaji Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Juma
Baada ya kuapishwa Rais Magufuli amewataka Mawaziri hao kuanza kazi mara moja, na wamebadilishana nyaraka mbali mbali za wizara ambazo walikuwa wanatumikia awali, kwa wale ambao wamehamishwa wizara.

No comments: