Mbwembwe za Yanga baada ya kutua kagera



Klabu ya Yanga inatarajiwa kuanza safari siku ya alhamisi kuelekea mkoani Kagera ambako itacheza mchezo wa ligi kuu dhidi ya Kagera Sugar kabla ya kusfiri kuelekea Mkoani Shinyanga ambako itamenyana na klabu ya Stand United.
Yanga ambayo kwa sasa inashikilia nafasi ya 6 hukuikiwa na pointi 9 nyuma ya Tanzania Prisons, inatarajiwa kutua Mkoani Kagera kwa Ndege kesho asubuhi huku ikijumuisha wachezaji wote isipokua kiungo Mzimbabwe Thabani Kamusoko.
Kwa mujibu wa kiongozi mmoja kutoka katika klabu hiyo amesema kua Kamusoko atakua nje ya uwanja kwa kipindi kisichopungua wiki mbili.
Yanga itacheza mchezo wake wa kwanza Mkoani Kagera dhidi ya Wakata Miwa wa Mkoa huo Kagera Sugar siku ya Jumamosi 14/10/2017 katika mtanange utakaopigwa uwanja wa Kaitaba.
Pata habari za Michezo kiganjani mwako kwa kudownload hapa.

No comments: