Msanii wa Hip Hop nchini Bill Nass
MSANII wa Hip Hop nchini Bill Nass anayetamba na wimbo wake mpya wa Sina Jambo amefunguka juu ya upendo wake kwa msanii mwenziye ambaye anafahamika kwa jina la Nandy, akisema ana vigezo vyote vya kuitwa mke wake.
Bill Nass amesema kwa sasa hana mpango wa kuoa, pia amefunguka na kusema kuwa hata muda ukifika bado atakuwa na vigezo vyake anavyovizingatia.
”Sijakaa nikafikiria suala la kuoa kwa sababu mimi nina vigezo vyangu ambavyo nataka, najua namtaka mwanamke wa aina gani. Kwanza suala la kuoa kwangu limenipitia mbali sana, sifikirii kuoa kwa sasa.”
Alipoulizwa kuhusu mtu ambaye anaona anelekea kidogo kuwa mke wake, alimtaja Nandy.
“Kiukweli kabisa katika hili suala la kumtaja ni zito lakini ni hivi, Nandy nimemuona ana asilimia sitini za kuolewa na mimi, kwa sababu ana vigezo vyote ambavyo navitaka,” alisema Bill Nass.
Tetesi zinazoendelea ni kwamba Bill Nass na Nandy wapo kwenye mahusiano lakini hawataki watu wayafahamu mahusiano yao.
No comments: