Meneja wa klabu ya Manchester United, Jose Mourinho kupitia mahojiano maalum na chombo cha habari cha Sky amesema timu yake ni bora zaidi kuliko ya Liverpool.
Mourinho ameyasema hayo wakati timu yake inaelekea katika mchezo mgumu wa Ligi Kuu nchini Uingereza dhidi ya Liverpool siku ya Jumamosi.
Zipo timu chache ambazo mreno huyo amepata tabu ya kupata matokeo wakati akicheza nazo zaidi Liverpool.
Ubingwa wake wa kwanza katika soka la Uingereza aliupata dhidi ya Liverpool mwaka 2005 ambao ni wa League Cup, na miongoni mwa pointi 28 za ligi alizipata kutoka kwa wapinzani wake hao wakati akiwa na Chelsea.
No comments: