Tambwe, Chirwa wapofiti Kwa Hili...

Klabu ya Young Africans inatarajia kuondoka hapo kesho asubuhi kwenda Bukoba tayari kujiwinda na mchezo dhidi ya Kagera Sugar utakaofanyika siku ya Jumamosi.


Mkuu wa habari wa klabu hiyo, Dismas Ten amesema wachezaji wote wako tayari kwa mchezo huo akiwemo Amissi Tambwe aliyekuwa akisumbuliwa na majeraha kwa kipindi kirefu.
“Timu imefanya mazoezi jana na leo Jumanne kwaajili ya maandalizi ya mchezo huo. Kesho timu itaondoka asubuhi kwenda Bukoba tayari kwa mchezo huo.” Amesema Ten.
Mkuu huyo wa kitengo cha mawasiliano cha Yanga ameongeza kuwa “Wachezaji wote wako vizuri na tunafurahi kuwa Tambwe amerejea na atakuwemo ingawa maamuzi ya kucheza au kutokucheza yatabaki kwa kocha, pia Obrey Chirwa naye yupo fiti.”
Yanga itaingia katika mchezo huo siku ya Jumamosi huku ikiwa na kumbukumbu ya ushindi mnono wa mabao 6-2 katika mchezo uliyopita wa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu uliyomalizika.

No comments: