msim wa pili wa kiswahili wazinduliwa rasim


Kampuni ya Star Media (T) Ltd, mmiliki wa nembo ya StarTimes inayotoa huduma za Matangazo ya kidigitali kote nchini, imezindua rasmi msimu wa pili wa shindano la kuingiza sauti za Kiswahili katika tamthiliya mbalimbali zenye lugha za kigeni.

Hafla ya ufunguzi ilifanyika tar 26 September katika hoteli ya Colosseum na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa Kiswahili wakiwemo viongozi wa BAKITA na wahadhiri wa somo la Kiswahili kutoka chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Kuanza kwa msimu huu ni mwendelezo wa Shindano hilo lililofanyika kwa mara ya kwanza mwaka jana na kufikia mikoa mitatu Tanzania Bara na Visiwani. Akizungumza nasi Meneja Mahusiano wa kampuni hiyo Ndg. Juma Suluhu alisema “Mwaka huu tumefanya mabadiliko makubwa katika Shindano hili, kubwa la kwanza ikiwa ni kuongezeka kwa Mkoa mwingine ambao utafikiwa na Shindano hili. Mwaka jana tulifanya Zanzibar, Dar es Salaam na Arusha lakini mwaka huu tutafika hadi Mwanza”.

“Wakazi wa kanda ya ziwa kwa mwaka huu watapata fursa ya kushiriki na kushinda Shindano hili adhimu kabisa ili kuweza kuwa mabalozi wa Kiswahili duniani kote, pia tumeongeza muda wa usaili kutoka ilivyokuwa Siku moja mwaka jana na sasa usaili utafanyika kwa siku mbili kwenye mikoa iliyotajwa ili kutoa fursa kwa watu wengi zaidi kushiriki”, aliongeza Juma.

Mwaka jana walipatikana washindi kumi ambao kwa pamoja wamepata mikataba ya kufanya kazi na Kampuni ya StarTimes, Beijing China. Mbali na kuajiriwa washindi hao wamepata fursa ya kushiriki midahalo mbali mbali ya kimataifa ukiwamo ule wa One Belt One Song ambao hukutanisha washiriki kutoka tamaduni kubwa duniani, hivyo washindi hawa walikuwa na nafasi ya kukitangaza Kiswahili katika hatua hiyo kubwa kabisa.

Mchunguzi wa Lugha Baraza la Kiswahili la Taifa,Mussa Kaoneka akizungumza wadau waliohudhuria katika hafla ya uzinduzi wa shindano la kuingiza sauti.

“Siyo tu kwamba washiriki hupata nafasi nzuri za ajira bali pia hupata nafasi ya kuwa mabalozi wazuri wa lugha ya Kiswahili na utamaduni wa Kitanzania, nitoe wito kwa watanzania wengi zaidi kujitokeza kushiriki” alisema Juma.

Kampuni ya Star Media (T) Ltd pia imepongezwa kwa jitihada zake za kuimarisha mahusiano na watanzania. “StarTimes imekuwa mdau mkubwa wa uchangiaji maendeleo hasa kupitia vipaji na sasa tutashuhudia watanzania wenzetu wengine wakienda kufanya kazi nje, wanapata ajira na kukitangaza kiswahili”.


Mhadhiri wa Taasisi ya Taaluma za Kiswahili Chuo Kikuu cha Dar es salaam,Dkt.George Mrikaria akizungumza wadau waliohudhuria katika hafla ya uzinduzi wa shindano la kuingiza sauti.

Aidha Juma alieleza kwamba Shindano la mwaka huu litakuwa na mvuto wa aina yake kwani litahusisha utoaji wa Burudani mbali mbali litakapokuwa likiendelea, pia washindi wa mwaka jana wanatarajiwa kutua nchini ili kutoa mbinu kadha wa kadha kwa washiriki watakaoingia hatua ya fainali.

Usaili wa kwanza utafanyika visiwani Zanzibar Jumamosi hii tarehe 30 Septemba na baadaye tarehe 8 Oktoba, Usaili utahamia Mwanza kabla ya kurejea Dar es Salaam tarehe 14 Oktoba. Kwa wakazi wa mikoa ya jirani na iliyotajwa ni vyema wakasogea kwenye mikoa husika kwa tarehe zilizotajwa.

Shindano la vipaji vya kuingiza Sauti litakuwa likionyeshwa moja kwa moja kupitia Chaneli ya St Swahili katika king’amuzi cha StarTimes. Hii pia ni nafasi nyingine kwa kampuni zitakazopenda kujitangaza, kutumia nafasi hii ya kipekee kutangaza na StarTime

No comments: