Neno la Didie Drogba la sisimua wengi

Nyota wa zamani wa Ivory Coast na Chelsea Didie Drogba amempongeza winga wa Liverpool na Misri Mohamed Salah baada ya kuisaidia timu yake ya taifa kufuzu fainali za kombe la dunia 2018 nchini Urusi.
Salah alifunga mabao mawili kwenye mchezo wa Kundi E kuwania kufuzu kombe la dunia kutoka Afrika dhidi ya DR Congo jana usiku.
Drogba ametumia ukurasa wake wa mtandao wa Twitter kumpongeza Salah ambapo ameandika, “Hongera kaka yangu, Najivunia wewe, umekuwa kiongozi bora kwenye taifa lako, umenikumbusha mimi na Ivory Coast mwaka 2006”.
Baada ya ushindi wa jana Misri, imefikisha alama 12 na kufanya iwe timu ya pili kufuzu kombe la dunia 2018 kutoka Afrika baada ya Nigeria.
Hii ni mara ya kwanza kwa Misri kufuzu fainali za Kombe la dunia baada ya miaka 28 kupita ambapo mara ya mwisho ilikuwa ni mwaka 1990 wakati huo Mohamed Salah hajazaliwa

No comments: