Msanii Nay wa Mitego amesema mvutano wa Diamond ana Alikiba haujaathiri wimbo wake hata mmoja.
Nay ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma Makuzi ameiambia Dj Show ya Radio One kuwa kipimo cha ngoma zake kufika mbali ni pale anapokuwa kwenye show au mapokezi ya watu mtaani ila mambo ya mtandaoni hayaathiri chochote.
“Ni wimbo wangu gani umeathiriwa na ugomvi na Diamond na Alikiba?” alihoji Nay wa Mitego.
“Majibu ya wimbo unayapata kwenye show, majibu ya wimbo unayapata mtaani, mimi nafanya muziki kwa ajili ya watu wangu wa mtaani siyo watu wa kwenye mitandao” amesema.
Ameongeza kuwa nguvu yake ya mtandaoni anaijua na nguvu yake ya mtaani anaijua, hivyo majibu sahihi yanayothibitisha ukubwa wa wimbo wake ni pale anapokuwa kwenye show jinsi watu wanakuwa wanaimba na kupokea.
No comments: