Mechi ya Simba na Yanga inayotarajiwa kupigwa Oktoba 28, inatajwa huenda ikachezwa Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Awali, kulikuwa na maombi kutoka Yanga kwamba mechi yao dhidi ya Simba ikachezwe sehemu nyingine tofauti na Dar es Salaam, hata hivyo taarifa zilizopo ni kwamba Bodi ya Ligi haijakubaliana nazo kwa hiyo mechi itachezwa palepale Uwanja wa Uhuru.
Mtendaji Mkuu Bodi ya Ligi, Boniface Wambura alisisitiza kwamba “Uamuzi wa bodi umezingatia kanuni ya sita (kanuni ndogo ya sita) kuhusu uwanja ambapo mamlaka ya mwisho kuhusiana na mechi kuhama au haihami inabaki kwa bodi ya ligi na TFF.”
Timu hizo zinatarajiwa kukutana Oktoba 28 kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara huku Yanga ikiwa na kumbukumbu kuikosa Ngao ya Jamii iliyonyakuliwa na Simba msimu huu.
No comments: