Hili ndo kosa la Simba



Kamati ya Bodi ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi imeipiga faini klabu ya Simba sh 500,000 (laki tano) kwa kosa la kuingia uwanjani kwa kutumia mlango usio rasmi katika mechi dhidi ya Mbao FC iliyofanyika Septemba 21 Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza.
Simba imevunja Kanuni ya 14(14) ya Ligi Kuu, na adhabu dhidi yao ni kwa mujibu wa Kanuni ya 14(49) ya Ligi Kuu. Pia Kamishna wa mechi hiyo, Maliki Tibabimale amepewa Onyo Kali kwa kutoripoti kitendo hicho cha Simba.
Kwa upande mwingine kamati imeiadhibu Singida United sh. 500,000 (laki tano) kutokana na mashabiki wa timu hiyo kuingia uwanjani kushangilia ushindi baada ya mechi dhidi ya Kagera Sugar iliyofanyika Septemba 23 mwaka huu Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.
Wakati huo Stand United imepigwa faini ya jumla ya sh. 1,500,000 (milioni moja na laki tano) kutokana na makosa mawili kwenye michezo miwili tofauti ambayo ni Wachezaji kuvaa jezi zenye namba tofauti na zilizosajiliwa kwenye mechi dhidi ya Simba pamoja na mashabiki wake kufanya vurugu kwenye mechi dhidi ya Mbeya City na Simba.
Kamati imeionya klabu ya Stand United endapo vitendo hivyo vitatokea tena haitasita kuichukulia hatua kali zaidi za kikanuni. SIMBA YAKUTANA NA RUNGU LA BODI YA UENDESHAJI LIGI NI BAADA YA KUFANYA KOSA HILI

No comments: