Jinsi ya kupika Ubuyu

Mahitaji.
1. Sukari vikombe 2
2. Maji vikombe 2
3. Nusu kikombe unga wa ubuyu
4. Vikombe 4 ubuyu wenyewe
5. 1/4 pili pili ya unga
6. 1/4 tsp chumvi
7. 1/4 tsp iliki ya unga
8. Rangi nyekundu au yeyote ile utakavyopenda.

Namna ya kufanya.
1. Katika sufuria,weka maji na sukari na chumvi na pili pili ya unga na Rangi na iliki. Moto uwe juu kiasi na changanya vyote hivyo vipike vizuri.

2. Wakati vitu vinaanza kujipika utakuta rojo linatoa mapovu. Endelea tu kukoroga acha rojo lipikike vizuri. Baada ya hapo mapovu yakianza kutulia inamaanisha kua rojo limeanza kua zito.

3. Sasa hapo chota kidogo katika mwiko na test kwa vidole kama rojo linanata ua halinati. Rojo linatakiwa linate ndio linakua limeiva. Lisinate San kiasi tu.

4. Kisha mimina ubuyu wa kokwa na changanya vizuri kabisa katika rojo. Endelea kupika vizuri kama dakika 2 hivi. Kisha mimina unga wa ubuyu na changanya vizuri tena.

5. Endelea kupika mpaka unaona sukari inaanza kuganda na kung'aa na kushika vizuri katika ubuyu. Hapo sasa zima jiko na mimina ubuyu katika sinia kubwa na acha ubuyu upoe.

Ukishapoa ubuyu tayari kuliwa.

No comments: