Waafrika wanaowania Ballon d’Or 2017

Miongoni mwa majina 30 yaliyotajwa hapo jana kuwania tuzo kubwa kabisa ya mchezo wa soka duniani Ballon d’Or 2017 wapo wachezaji wawili wanaochezea timu za taifa za Afria.
Orodha hiyo iliyotolewa jana siku ya Jumatatu na France Football imewataja, Sadio Mane ambae ni kiungo wa timu ya taifa ya Senegal na klabu ya Liverpool inayoshiriki Ligi Kuu nchini Uingereza.
Mane ameingia uwanjani mara 99 katika michezo yote ya Ligi Kuu nchini Uingereza akiwa na klabu yake ya zamani ya Southampton pamoja na timu yake ya sasa ya Liverpool.


Kiungo huyo kutoka Senegal amefunga jumla ya mabao 37 na kutoa pasi zilizochangia mabao ‘Assists’ mara 14 katika michezo yote hiyo aliyocheza akiwa katika timu hizo mbili.
Mchezaji wa pili aliyetajwa katika orodha hiyo ni Pierre-Emerick Aubameyang ambae anakipiga katika timu ya taifa ya Gabon na klabu ya Borussia Dortmund inayoshiriki ligi ya Bundesliga nchini Ujerumani ikiwa chini ya meneja Peter Bosz.

NEYMAR, DYBALA NA KANTE WATAJWA KUWANIA BALLON D’OR 2017
Mpaka sasa tayari majina ya wachezaji 30 yamesha tajwa na hawa ndiyowachezaji wanao wania tuzo hiyo ya Ballon d’Or 2017.
Neymar (PSG/Brazil)
Luka Modric (Real Madrid/Croatia)
Paulo Dybala (Juventus/Argentina)
Marcelo (Real Madrid/Brazil)
N’Golo Kante (Chelsea/France)
Luis Suarez (Barcelona/Uruguay)
Sergio Ramos (Real Madrid/Spain)
Jan Oblak (Atletico Madrid/Slovenia)
Philippe Coutinho (Liverpool/Brazil)
Dries Mertens (Napoli/Belgium)
Kevin De Bruyne (Manchester City/Belgium)
Robert Lewandowski (Bayern Munich/Poland)
David De Gea (Manchester United/Spain)
Harry Kane (Tottenham/England)
Edin Dzeko (Roma/Bosnia)
Antoine Griezmann (Atletico Madrid/France)
Toni Kroos (Real Madrid/Germany)
Sadio Mane (Liverpool/Senegal)
Radamel Falcao (Monaco/Colombia)
Gianluigi Buffon (Juventus/Italy)
Lionel Messi (Barcelona/Argentina)
Mats Hummels (Bayern Munich/Germany)
Edinson Cavani (PSG/Uruguay)
Pierre-Emerick Aubameyang (Borussia Dortmund/Gabon)
Karim Benzema (Real Madrid/France)
Eden Hazard (Chelsea/Belgium)
Kylian Mbappe (PSG/France)
Cristiano Ronaldo (Real Madrid/Portugal)
Isco (Real Madrid/Spain)
Leonardo Bonucci (Juventus/Italy)
Sherehe za tuzo hizi zinatarajiwa kufanyika mwezi ujao Jijini London

No comments: