Wanawake ruksa kuendesha magari Saudia


Mfalme Salman wa Saudi Arabia ametoa idhini ya wanawake kuendesha magari,hii ikiwa ni kwa mara ya kwanza katika historia ya taifa.Uamuzi huu umefikiwa kutokana na harakati za muda mrefu kwa makundi ya wanawake na haki za bindamu kushinikiza wanawake waruhusiwe kuendesha magari.

Kwa muda mrefu Saudi Arabia imekuwa nchi pekee Duniani kuwazuia wanawake kuendesha magari. Abdallah al-Mouallimi Mwakilishi wa umoja wa mataifa kutoka Saudia ametangaza habari hizi umoja wa huko umoja mataifa.

"Ndugu Mwenyekiti,Mabibi na mabwana.Najua mtapenda kujua jambo hili kwamba dakika chache zilizopita Mfalme amepitisha sharia inayowapa idhini,wanawake nchini Saudia kuendesha magari.Hii ni historia mpya leo kwa jamii ya Saudia,kwa wanaume na wanawake.Na kwa sasa tunaweza kusema kitu angalau.'' Abdallah al-Mouallimi.

Akizungumza na waandishi wa msemaji wa idara ya Marekani,Bi.Heather Nauert amelezea kupokea kwa furaha tangazo hilo.

No comments: