Msanii wa muziki kutoka RockStar4000, Ommy Dimpoz amedai starehe yake kubwa katika maisha yake ni kutembea katika mataifa mbalimbali duniani.
Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo wake mpya, Cheche amefunguka kwa kusema watu wasimshangae kwanini anasafiri sana kwani hiyo ndio starehe yake kubwa katika maisha yake.
“Mimi ni msanii ambaye sivuti sigara wala sinywi pombe lakini starehe yangu kubwa ni kutembea, napenda sana,” alisema Ommy Dimpoz. “Kwahiyo kama unaona sijasafiri kwa show basi tambua kuna kitu anaenda kufanya au ni kwasababu ya starehe zangu,”
Aliongeza,”Kwahiyo ile hela ambayo nilikuwa niipeleke kwenye pombe mimi naidunduliza kwaajili ya kufanya kile ambacho mimi nakipenda, na mimi naona ni sahihi lakini tatizo la watanzania wanakupigia hesabu ya kila kitu unachokifanya na wanaona ni gharama kubwa sana kumbe sio ni kujipanga tu,”
No comments: