Video: IGP Sirro upinzani tunaachaje kumjadili Lissu? – Chadema



Chama cha Demokrasia na Maendelo (Chadema), kimemtaka Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro kufanya upelelezi na kuhakikisha wanawatia nguvuni walioshiriki katika tukio la kumshambulia Mbunge wa Singida Mashariki, na si kuwataka watu wasilizungumzie hilo suala.
Akizungumza na wanahabari leo, Mwanasheria wa chama hicho, John Mallya amesema aliyepigwa risasi zaidi ya 30 pale Dodoma hakuwa ni mbuzi ni mtu kwanini tusimjadili? alihoji Mwansheria huyo.
“Polisi anaanza kujadili raia au kuamuru raia Mamlaka hayo hana mamlaka hayo kwenye sheria wala kwenye kanuni wakati huo ambapo wanasiasa wana sheria wanannchi ambayo jimbo Mhe. Lissu anatoka wanajadili juu ya muhtabali wa mtu ambaye anawahusu Kamanda sirro anapaswa yeye anyamaze, kama kuna mtu wakunyamaza hapa si wanasiasa ni Sirro.IGP anyamaze afanye kazi ya upelelezi lakini kuwaambia watu watu wanyamaze kwenye mitandao ya kijamii na vijiwe wanavyozungumza ni kinyume na sheria na ana kiuka ibara ya 18 ya Katiba na anafanya tukose imani zaidi na jeshi la polisi ambalo kwa kweli wameanza kupoteza imani hiyo,” Alisema Mallya.
“Angeweza kufanya hivyo kama mtu anaehusika na jambo hili pengine ni askari wake angekuwa amepigwa risasi kama ambazo Mhe. Tundu Lissu alipigwa angeweza kuamaru askari wenzie wasijadili, kwakuwa aliepigwa ni Mwanasiasa Tundu Lissu ni mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Tundu Lissu ni Rais wa Chama cha Mawakili, Tundu Lissu ni mwanasheria Mkuu wa Chama cha upinzani unaachaje kumjadili? Aliyepigwa risasi zaidi ya 30 pale Dodoma hakuwa ni mbuzi ni mtu kwanini tusimjadili,” Aliongeza Mallya.
“Ikumbukwe kabla ya kupiga marufuku huko Mbeya katika ziara hizi anazoendelea nazo alisema anaejua taarifa za wahalifu ampelekee sasa taarifa hizo tutapashanaje habari bila kuzungumza,” alihoji.

No comments: