Rais wa Marekani, Donald Trump amekumbana na mistari 11 ya matusi kutoka kwa rapa, Eminem ambaye ametoa wimbo maalumu aliouita Came to Stomp.
Eminem alighani mistari hiyo ya dakika 4.5 katika utoaji wa tuzo za muziki za BET zilizotolewa jana Jumanne nchini Marekani.
Hii si mara ya kwanza kwa Eminem kumkosoa Trump isipokuwa amekuja kivingine. Wakati wa uchaguzi mwaka jana, Eminem alighani mashairi ya kuwatusi mashabiki wa Trump lakini sasa amekwenda hatua moja akimwita ‘Babu Mbaguzi’ na majina mengine ambayo ni matusi ya nguoni.
Katika moja ya mashairi yake anasema Trump ni mbaguzi na mchokozi ambaye anaweza kuanzisha vita ya nyuklia lakini akakimbilia juu na ndege yake mpaka mabomu yatakaposimama kurushwa.
“Ni askari ambaye ataanzisha vita lakini atajaza mafuta katika ndege na kukimbilia anga la juu akiwaacha watu wakifa,” anaghani Eminem.
Katika mstari mwingine anamtusi Trump kwa kupenda kushindana na watu wanaompinga kwa mabishano katika mtandao wa Twitter na kuwapuuza wananchi wanaoteseka baada ya maeno mbalimbali ya nchi hiyo kukumbwa na kimbunga.
Katika mstari wa mwisho Emimen anasema wanaipenda nchi yao na jeshi lakini wanamchukia Trump.
No comments: