Taarifa kutoka kunako Klabu ya Simba ni kua baada ya mapumziko mafupi ambayo kikosi cha Simba kilipewa pamoja na kuwapa nafasi baadhi ya wachezaji kwenda kwenye majukumu ya Timu za Taifa wanazoziwakilisha, kikosi cha Simba leo kinatarajiwa kuanza mazoezi rasmi kujiandaa na muendrlezo wa ligi kuu Tanzania bara.
Simba ambayo inatarajiwa kushuku dimbani kumenyana na klabu ya Mtibwa Sugar katika mchezo wa logi kuu utakaopigwa katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es salaam siku ya jumapili ya tarehe 15.10.2017
Katika kuelekea mchezo huo klabu hizo zinakumbu kwa klabu ya Simba kuibuka na ushindi katika mchezo wake wa mwisho wa ligi ilioucheza Shinyanga dhidi ya Stand United wakati huo klabu ya Mtibwa yenyewe katika mchezo wake wa mwisho wa ligi iliambulia sare tasa dhidi ya bingwa mtetezi wa ligi hiyo Yanga sc.
No comments: