Mwanaume aliyelipa mil. 50 kubadilisha sura awe kama mwanamke akimbiwa na madaktari baada ya upasuaji kufeli

Mwanamme mmoja nchini Colombia aliyetambulika kwa jina la Jerson Trujillo, amejikuta akiugulia maumivu ya kujitakia baada ya kukimbiwa na madaktari uchuro waliomhadaha kuwa wanauwezo wa kumbadilisha sura.


     Jerson Trujillo
Jerson Trujillo (28) amesema alitaka kuwa kama mwanamke lakini madaktari hao ambao walisema wanauwezo wa kufanya hivyo walishindwa kutimiza lengo la kijana huyo.
Taarifa kutoka kwenye mtandao wa BBC Mundo zinaeleza kuwa kijana huyo alifanyiwa operation hiyo miaka minne iliyopita lakini miaka yote uso wake umekuwa ukibadilika badilika na kuvimba kitu ambacho kina mfanya ahudhurie kila siku hospitalini.
“ Nilitaka kubadilisha uso wangu ili niwe na muoekano wa kike miaka minne iliyopita lakini tangu hapo uso wangu umekuwa umomonyoka kila siku, Nimetafuta madaktari wengine lakini nao wamekuwa wakishindwa kunitibu na kubaki na maumivu makali kila siku, Najutia kwa maamuzi yangu, “amesema Trujillo kwenye mahojiano yake na BBC Mundo .


Jerson Trujillo kabla ya kubadilisha sura
Hata hivyo amesema kadri muda unaavyozidi kwenda anaona maumivu yaazidi kuongezeka na mbaya zaidi hata muonekano unabadilika.
“ Sikuwa na sura mbaya kivile ila nilitaka niwe kama mwanamke kabisa lakini ndio nimekutwa na haya mpaka sasa wazazi wangu wamenilipia zaidi ya shilingi milioni 50 kunusuru uso wangu ila bado hali haiimariki, “amesema Trujillo.
Hata hivyo, Trujillo amesema aliaminishwa kuwa upasuaji huo ungeenda salama lakini mambo yaligeuka na kukimbiwa kabisa na madaktari hao ambao amesema walikuwa wanatumia visu.
Kwa mujibu wa tafiti kutoka Chama cha Madaktari wanaojihusisha na upasuaji mdogo wa kubadilisha mwili wa binadamu ( Spanish Society of Plastic, Reconstructive and Aesthetic Surgery) kutoka Hispania wamesema ni asilimia 16 tu ya watu wote wanaofanyiwa mabadiliko ya miili yao barani Ulaya ndio hufanikiwa lakini wengi upasuaji wao unaenda ndivyo sivyo.

No comments: