Mshambuliaji wa Manchester United, Romelu Lukaku anasumbuliwa na maumivu ya kifundo cha mguu na kuna uwezekano akaukosa mchezo wa timu yake ya taifa ya Ubelgiji dhidi ya Bosnia.
Lukaku amefanyiwa vipimo kujua ukubwa wa tatizo la afya yake na bado haijajulikana kama ataweza kucheza wiki hii katika majukumu yake ya timu ya taifa au la.
Straika huyo yupo katika kiwango kizuri ambapo amefunga mabao 15 katika mechi 12 zilizopita akiwa akwenye timu ya taifa na klabu, inaaminika alipata maumivu hayo Jumamosi iliyopota wakati United ilipocheza dhidi ya Crystal Palace.
Alipoulizwa juu ya mchezaji huyo kuitumikia timu ya taifa au apumzishwe, Kocha wa United, Jose Mourinho aligoma kuzungumia suala hilo kwa kusema kuwa anaamini hilo ni jukumu la kocha wa timu ya taifa ya Ubelgiji.
Ugonjwa huo umesababisha hofu kubwa kwa mashabiki wa United ambao wanamtegemea mchezaji huyo kuwa ndiyo jembe lao kwa sasa.
No comments: