Kwa sasa vipo vyakula vingi sana ambavyo vimekuwa na sukari na tunavitumia karibu kila siku. Kwa bahati mbaya au nzuri vyakula hivi vya sukari vimekuwa vikipendwa na wengi bila ya kujali madhara yake kiafya yakoje.
Wengi wetu hatujui sana kiundani hasa pale tunapotumia vyakula vingi vya sukari, ni madhara gani ambao yanaweza kukutokea zaidi, tumekuwa tukijua juu juu tu kwamba ukila vyakula vya sukari vinaweza kukuletea shida hii au ile bila kuwa na uhakika sana.
Kwa sababu hiyo ndani ya makala haya ya afya, tutakueleza kinagaubaga sababu ya msingi ni kwa nini unatakiwa uache kutumia sukari kwa wingi mwilini mwako na ikiwezekana kuacha kabisa baadhi ya matumizi ya vitu vyenye sukari nyingi sana.
1. Sukari nyingi mwilini ni kisababishi cha magonjwa.
Matumizi ya sukari kwa wingi ni chanzo kimojawapo cha kuongezeka kwa uzito, lakini si hivyo tu sukari inapokuwa nyingi mwilini inaweza kukupelekea kupata magonjwa kama vile magonyjwa ya moyo na kuongezeka kwa shinikizo la damu jambo ambalo ni hatari kwa afya yako kwa kiasi kikubwa.
2. Sukari nyingi mwilini inapunguza uwezo wa kuona.
Mara nyingi wanaoutumia sukari kwa wingi sana au wale amabao viwango vya sukari vimeongezeka mwilini mwao, moja ya madhara yake kwa baadae ni kutokuona vizuri. Hilo hutokea kwa sababu, sukari inapokuwa nyingi hupelekea lensi ya jicho kuongezeka na matokeo yake matatizo ya macho huanza kujitokeza kwa mhusika.
3. Sukari nyingi huozesha meno.
Bila shaka hili umeshawahi kulisikia au kuliona. Na mara nyingi hutokea sana kwa watoto, meno huweza kuoza baada ya matumizi ya sukari kwa wingi. Kinachotokea sukari huzalisha bakteria wenye sumu ambapo hao huweza kuharibu meno na kupelekea kuweza kuoza kabisa.
4. Sukari nyingi inapoteza uwezo wa mwili kukabiliana na magonjwa.
Wale wote ambao sukari inakuwa imeongezeka miili yao inakuwa haina uwezo wa kukabiliana na magonjwa. Unajua ni kwa nini? iko hivi,.. unapokuwa na sukari nyingi mwilini inatabia ya kuua seli nyeupe ambazo husaidia kupambana na magonjwa. Kwa hali hiyo ndio maana watu wenye visukari hawaponi vidonda kwa sababu kama hii.
5. Sukari nyingi mwilini zinasababisha mwili kuonekana umeezeka.
Kila sukari inapokuwa nyingi mwilini, inazalisha kemikali ambazo baadae kemikali hizo hupelekea mwili wako kuanza kuoneana kama vile umezeeka. Hapa njia pekee ya kuondokana na hali hiyo ni kupunguza matumizi ya sukari. Vinginevyo utaanza kuonekana kikongwe.
6. Sukari nyingi husababisha viungo vya mwili kulegea.
Zipo ‘joints’ kama vile za miguu hasa pale unapokuwa unatembea zinakuwa zinachoka upesi na kulegea kama mwili wako una sukari nyingi. Hali hii hutokea sana hasa kwa wagonjwa wenye kisukari. Hii ninhali ambayo huwakuta wengi wagonjwa wa kisukari na inakuwa ni hali inayosumbua.
Mwisho kabisa hapa sina shaka mpaka unafika mwisho wa makala haya utakuwa umeelewa hatua za kuchukua na hiyo haitoshi ni vyema ukamshirikisha na mwingine makala haya ili aweze kujifunza na kundokana na matatizo ambayo pengine yangemkuta.
No comments: