Kama Utaitumia Nguvu HiI, Ndiyo Itakayokufanya Ufanikiwe

Kwa nguvu ya ung’anga’nizi, ndiyo inayopelekea tone moja la maji linalodondoka kila siku ipo siku livunje jiwe hilo kabisa.

Kwa nguvu ya ung’ang’anizi, mbegu dogo kabisa inauwezo wa kukua kwenye tawi la mti mkubwa na hatimaye kuwa mti mkubwa sana pia.

Kwa nguvu ya ung’ang’anizi kila mtu ana uwezo wa kubadilisha maisha yake, hata kama mtu huyo yupo kwenye wakati mgumu sana.

Kwa nguvu ya ungang’anizi, ndiyo inayofanya maisha ya wengine yawe mazuri na maisha ya wengine kuwa mbaya kutokana na kung’ang’ania vibovu.

Kwa nguvu ya ung’ang’anizi, ndio inayompa mtu mafanikio hata kama anatokea chini kabisa bila kuwa na kitu.

Hakuna kinachoshindikana, hakuna mafanikio ambayo utashindwa kuyapata kama kweli leo, utaamua kung’ang’ania kile unachokitaka kwenye maisha yako.

Nguvu unayotumia kung’ang’ania mambo, hata kama nguvu hiyo ni kidogo itakusaidia sana kufanikiwa kwa kiasi kikubwa.

Watu wengi wanashindwa kufanikiwa sana, kwa sababu ya kushindwa kutumia nguvu ya ung’ang’anizi kwenye yale mambo wanayoyafanya.

Sio ajabu sana kumkuta mtu kaanzisha jambo leo, lakini kesho mtu huyo akikutana na changamoto anaacha kila kitu.


Huwezi kufanikiwa kwa viwango vikubwa kama wewe si king’ang’anizi. Kama mafanikio kweli  utayapata, lakini utapata mafanikio ya rasharasha.

Unatakiwa utambue hata ukutane na changamoto, unatakiwa kukomaa mpaka kieleweke. Hakuna mafanikio yanayokuja kirahisi.

Ikiwa kuna kitu unakifanya hata sasa na unaona hakikupi matokeo ya upesi kama unavyotaka, jipe muda kwanza na usikimbilie kukata tamaa.

Kama utakuwa ni mtu wa kukata tamaa mapema na kushindwa kuwa king’ang’anizi basi elewa utashindwa kwenye mambo mengi sana.

Ifike mahali ujiulize ni wapi unapotaka kufika kimaisha, ni wapi unapotaka kwenda na ukishajua hivyo amua kabisa kung’ang’ania mpaka kieleweke.

Usikubali kitokee kitu eti ambacho kitakuzuia kufanikiwa kwako. amua kwamba iwe itakavyokuwa bila kujali utatumia muda gani mafanikio yako ni lazima.

Ukijivusha ujasiri huo wa kuwa king’anganizi mafanikio yeyewe yatakupisha na kutakuwa hakuna namna nyingine ya kukuzuia.

No comments: