THE SUN:
Jose Mourinho yupo tayari kusaini mkataba mpya wa miaka mitano wenye thamani ya Pauni Milioni 65 katika klabu ya Manchester United.
Arsenal wana hofu kwamba Alexis Sanchez hatokuwa tayari kucheza mechi dhidi ya Watford kutokana na maumivu ya kushindwa kufuzu kucheza kombe la Dunia nchini Urusi.
Crystal Palace wapo tayari kupigana vikumbo na Newcastle United kwa straika wa Besiktas Cenk Tosun.
THE DAILY TELEGRAPH:
Kiungo wa Chelsea N’golo Kante atakuwa nje ya dimba mpaka mwezi Novemba baada ya kuumia misuli ya nyuma ya paja.
DAILY MAIL:
Barcelona watawasilisha ofa ya awali ya Pauni Milioni 120 kwa kiungo wa Liverpool, Philipe Coutinho mwezi Januari.
Jose Mourinho amekasrika baada ya Romelu Lukaku kuchezeshwa mechi ya Ubeligiji dhidi ya Cyprus.
Arsenal wapo tayari kumharakisha kikosini beki Laurent Koscienly ili kuongeza nguvu bada ya Shkodran Mustafi
DAILY STAR:
Kocha wa Southampton Maurico Pellegrino anajiandaa kutoa ofa kwa Barcelona ili kumnasa straika wa klabu hiyo Paco Alcacer mwezi Januari.
Straika wa Newcastle Ayoze Perez amemshukuru kocha Rafa Benitez kwa kuokoa maisha yake ya soka.
Wilfried Zaha amesema kwamba yupo fiti kukabliana dhidi ya Chelsea wikiendi hii.
DAILY MIRROR:
Juan Mata yupo tayari kukataa ofa ya kuhamia China na badala yake kusaini mkataba mpya wa kubaki Manchester United.
West Brom wanataka kumsajili beki wa kushoto wa Inter Milan na timu ya taifa ya Japan Yugo Nagatomo .
THE TIMES:
Zlatan Ibrahimovic anatarajiwa kurejea kwenye mazoezi rasmi na kikosi cha Manchester United mwezi ujao na atakuwa tayari kucheza mwezi Desemba.
DAILY EXPRESS:
Mmiliki wa Sunderland Ellis Short yupo tayari kuiuza klabu yake kwa thamani sawa na ile ya nyumba yake ya Pauni Milioni 57.
No comments: