Rais wa Misri atoa zawadi hii baada ya wachezaji kufuzu World Cup 2018


Weekend iliyomalizika timu ya taifa ya Misri ilifanikiwa kufuzu kwenda kushiriki fainali za michuano ya Kombe la dunia nchini Urusi, kwa mara ya kwanza baada ya miaka 27, Misri wamefuzu kucheza fainali za kombe la dunia mwakani baada ya ushindi wa dakika za majeruhi wa magoli 2-1.
Magoli yote ya Misri dhidi ya Congo Brazzaville yalifungwa na staa wa Liverpool Mohamed Salah dakika ya 64 na dakika ya 95 kwa mkwaju wa penati hiyo ikiwa ni dakika chache zimepita toka Arnold Moutou asawazishe goli kwa Congo.
Ushindi huo umewafanya Misri wafuzu moja kwa moja kutokana na kufikisha jumla ya point 12 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote ile ya Kundi E lililokuwa na timu za Uganda, Ghana na Congo Brazzaville licha ya kila timu kusalia na mchezo mmoja.
Mara ya mwisho Misri kushiriki Kombe la Dunia ilikuwa mwaka 1990, miaka kabla ya Mohamed Salah kuzaliwa na zimepita fainali sita, hivyo kutokana na kiu ya muda mrefu Rais wa Misri Abdul Fattah al-Sisi ametoa zawadi ya dola 85,000 kwa kila mchezaji ambazo ni zaidi ya Tsh milioni 200 hiyo ni baada ya kukutana na kocha wao raia wa Argentina Hector Cuper.

No comments: