Petitman mume wa Esma Platnumz ambaye ni dada yake Diamond amelazimika kuvunja ukimya baada ya picha zinazomuonyesha akiwa na Mobetto katika hali ya mahaba.
Petit ambaye ni meneja wa Billnass na Country Boy, amedai picha hizo zimesambazwa kwa lengo la kumchafua yeye pamoja na familia yake.
“Picha zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii ni za zamani sana. Hazina uhusiano wowote na maisha yangu ya sasa au na yale yanayoendelea kuhusu Hamisa ambaye anaonekana pia katika picha hizo kwa sasa,” aliandika Petit Instagram.
Aliongeza,”Yeyote ambaye ameamua kuzisambaza ana nia moja tu. Kuniunganisha katika suala ambalo sihusiki na kunichafua. Mimi kwa muda mrefu niko na mke wangu mpendwa ambaye kila mtu anamjua na tuko busy kujenga familia yetu. Inawezekana jambo hili haliwafurahishi baadhi ya watu hivyo kuamua kusambaza picha za zamani kwa nia zao ovu. Niseme tu kwa kifupi hizo picha sio za kutilia maanani. Ni picha za zamani sana. Kwa sasa sio muda wa kuchafuana. Huu ni muda wa kila mmoja wetu kupambana kujijenga na kulea familia yake. Mimi kama baba wa familia jukumu langu ndio hilo”
Mobetto hivi karibuni amejifungua mtoto wa kiume, Abdul ambaye amezaa na muimbaji Diamond Platnumz.
No comments: