Aubameyang afunguka kuhusu usajili



Mshambulaji wa Borussia Dortmund Pierre-Emerick Aubameyang amesema klabu yake ipo tayari kumuuza muda wowote lakini yeye ndio anaamua kubaki.
Raia huyo wa Gabon amesema kuwa timu yake haijawahi kukataa kumuuza katika vipindi tofauti vya usajili vilivyopita lakini yeye ndio amekuwa akiweka ngumu kuondoka kwasababu anajisikia yupo nyumbani akiwa na timu hiyo.
“Ni kweli timu yangu tulikuwa tumekubaliana ipokee ofa kutoka klabu zinazohitaji huduma yangu lakini sikuondoka kwasababu najihisi nyumbani nikiwa Dortmund na huo ndio ukweli kuwa Borussia Dortmund ni familia yangu”, amesema Aubameyang.
Mkali huyo wa mabao ameongeza kuwa kwasasa hafikirii kwenda popote pamoja na uwepo wa ofa kutoka vilabu tofauti tofuati lakini anajiona ana jukumu la kuitumikia zaidi Dortmund.
Msimu uliopita Aubameyang mwenye miaka 28 alitwaa kiatu cha mfungaji bora katika ligi kuu ya soka ya Bundesliga na tayari msimu huu chini ya kocha mpya Peter Bosz ameshafunga mabao 13 katika michuano yote.

No comments: