Kiongozi wa Chama cha ACT- Wazalendo na Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe amesafirishwa na polisi kwenda Dodoma baada ya kutua uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwl Julius Nyerere kukamatwa akitokea Kigoma.Taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya ACT-Wazalendo, Mohamed Babu imesema Zitto amesafirishwa saa kumi usiku akitokea kituo cha polisi cha Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere (JNIA)kwenda Dodoma.
UPDATES: KUKAMATWA KWA ZITTO KABWE, KIONGOZI WA CHAMA ACT WAZALENDO:Kiongozi wa Chama Ndugu Zitto Kabwe amesafirishwa na polisi usiku huu (saa kumi) kutoka kituo cha polisi cha Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere, Dar es salaam kwenda Dodoma.Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Chama inafuatilia kwa umakini hatua kwa hatua kuhakikisha Usalama wake.
Tunawataka wanachama na wananchi kuendelea kuwa watulivu.Imetolewa tarehe 21 Septemba 2017
No comments: