Zari: Sitaki mtoto wa Mobetto ajipendekeze kwa wanangu

Image result for zari ze boss lady
Siku zote Tembo wakipigana zinazoumia ni nyasi! Hiyo imejidhihirisha kufuatia ‘vita ya penzi’ inayoendelea kuunguruma mitandaoni kati ya mwanamitindo Hamisa Mobeto na mfanyabiashara, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, ambao wote wawili wamezaa na mwanaume mmoja ambapo vita hiyo sasa wameihamishia kwa watoto, Zari ameibuka na kusema hataki kabisa ukaribu kati ya watoto wake na mtoto wa Mobeto.

PHOTO | COURTESY
Zari alifikia hatua ya kumtaka mtoto huyo akae mbali mita zisizohesabika na watoto wake, baada ya kuona ‘amewa-follow’ kupitia akaunti yake ya Instagram anayotumia jina la Prince Dylan, alilopewa na baba yake, ambaye ni mbongo Fleva.

Baada ya kitendo hicho, mashabiki hawakumuacha salama Zari. Wakamshushia kichambo cha mwaka huku wakimwambia kuwa ugomvi wao usiwahusishe watoto kwani hao watabaki kuwa ndugu milele na hakuna cha kubadilisha ukweli huo.

No comments: