Rais wa Ufilipino atoa ruhusa mwanae auawe kwa kosa la madawa ya kulevya


Ufilipino Rodrigo Duterte ameliambia jeshi la polisi nchini humo kufanya uchunguzi juu ya mwanaye wa kwanza Paolo Duterte, 42, anayetuhumiwa kuhusika na kikundi kikubwa cha uuzaji na uambazaji wa dawa za kulevya cha China na kuwaambia ushahidi ukionesha tuhuma hizo ni za kweli wamuue bila wasiwasi wowote.
Nchini Ufilipino katiba inaruhusu mtu yeyote anayejihusisha kwa namna yoyote na madawa ya kulevya auawe na hadi sasa watu zaidi ya 9,000 wameshauawa kutokana na makosa hayo.
Rais Duterte alimwambia mwanaye “amri yangu ni kuhakikisha wamekuua pindi itakapo thibitishwa unahusika na biashara hii ya dawa za kulevya, na nitawalinda mapolisi hao ambao watakuua.
Uliikosa hii? Serikali yalifungia Gazeti la MWANAHALISI

No comments: