Burundi yaridhika ufanisi, huduma bandari ya Dar es Salaam

Image result for bandari ya dar es salaam

Kampuni ya MINOLACS ya Burundi imeahidi kuendelea kuitumia Bandari ya Dar es Salaam baada ya kuridhika na ufanisi wa hali ya juu wa kuhudumia shehena ya ngano Tani 12,000 za kampuni hiyo hivi karibuni.


Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo Bw. Munir Bashir ameyasema hayo katika barua yake ya shukrani kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Mhandisi Deusdedit Kakoko ambapo pamoja na mambo mengine ameelezea jinsi Bandari ya Dar es Salaam ilivyo na ufanisi bora wa huduma.

“Tunashukuru sana menejimenti ya TPA na wafanyakazi kwa utendaji wenu mzuri na wa hali ya juu uliowezesha kuhudumia shehena yetu iliyoletwa na meli ya MV Loving,” imenukuu sehemu ya barua hiyo.

Akifafanua zaidi Mkurugenzi wa MINOLACS ameongeza kuwa, “…tunawashukuru sana na tunaaahidi kuongeza shehena kufikia tani 16,000 za ngano tutakazopitisha Bandari ya Dar es Salaam wiki ya kwanza ya mwezi Oktoba mwaka huu.”

MINOLACS ni Kampuni binafsi inayojishughulisha na biashara ya nafaka, kwa ajili ya chakula yenye uwezo wa mauzo ya kiasi cha Dola za Kimarekani Milioni 6.8 kwa mwaka. Tayari TPA imefungua huduma zake katika nchi ya Burundi, mji wa Bujumbura ili kusogeza huduma zake karibu na wateja. Pia ina ofisi zake mjini Lusaka- Zambia, Kampala, Uganda, Kigali-Rwanda na Lubumbashi nchiniJamhuri ya Kidemokrasia Kongo

No comments: