Muasisi wa Facebook Mark Zuckerberg anasema kuwa ataishirikisha Marekani matangazo 3,000 ya Urusi -yanayohusiana na siasa.
Ameahidi pia kwamba ataweka matangazo ya kisiasa katika hali ya uwazi zaidi kwenye mtandao wake katika siku zijazo.
" Tutashirikiana na wengine kubuni kiwango kipya cha uwazi wa matangozo yote ya kisiasa ya kwenye mtandao,"amesema Bwana Zuckerberg kwenye hotuba yake aliyoitoa kwenye mtandao wake wa Facebook.
Amesema kuwa matangazo ya kisiasa sasa yataonyesha wazi ni kampeni gani ama kampuni gani iliyoyalipia.
Ameongeza kusema kuwa kampuni yake inaendelea kuchunguza matukio ambayo watu wanatumia vibaya huduma ya matangazo ya biashara ya mtandao huo , ikiwemo Urusi pamoja na mataifa mengine.
Hatua ya kushirikisha taarifa wachunguzi imekuja baada ya shinikizo kubwa kutoka kwa umma ambao uliitaka Facebook kuwa na uwazi zaidi - na inaangaliwa kama jaribio la kampuni hiyo kuepuka kuwekewa masharti yoyote na serikali ya Marekani.
Mapema mwezi huu yalifichuliwa matangazo yenye uchochezi wa kisiasa ambayo yamekuwa yakiwalenga wapiga kura wa Marekani ,yaliyolipiwa , katika Facebook na Urusi ambayo yalionyesha kutumwa na watu wenye uhusiano na serikali ya Urusi.
Matangazo hayo hayakumuunga mkono mgombea fulani , Facebook ilisema, lakini badala yake kwenye matangazo hayo ulitumwa ujumbe wa taarifa za matusi kuhusu masuala muhimu , kama vile uhamiaji.
No comments: