Waziri afunguka wanyama waliochukuliwa Tanzania


Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Eng. Ramo Makani ametolea ufafanuzi suala la masalia ya mijusi mikubwa (Dinosaria) waliogunduliwa Tanzania na kuchukuliwa na wageni, na kusema kwamba serikali imefuatilia jambo hilo lakini haitaweza kuirudisha.

Akizungumza kwenye kipindi cha East Afrika Breakfast baada ya kuulizwa juu ya suala hilo, Injinia Makani amesema mifupa ya mijusi hiyo ni mikubwa sana kuisafirisha na pia imekaa 'delicate' sana, hivyo watafiti hao walishauri ni vyema waje wachimbe mingine ili ibaki hapa nyumbani, na sio kuirejesha mifupa hiyo.

Pia Injinia Makani amesema kuhusu masalia ya 'Dinosaria' waliogunduliwa mkoani Songwe hivi karibuni na kupewa jina la 'Songwenians shingopana', bado haijapata taarifa rasmi hivyo idara husika itafuatilia suala hilo.

No comments: