Kocha Mwingine Aachia Ngazi

64
Wimbi la makocha wanaovifundisha vilabu mbalimbali hapa nchini kuachiangazi limeendelea kua kubwa ambapo Asubuhi hii vyankende.com imepokea taarifa za kuachiangazi kwa aliekua kocha mkuu wa klabu ya Toto Africa Ya Mwanza,Almasi Moshi.

Taarifa inaeleza kua kocha huyo ameachia ngazi kutokana na klabu hiyo kutotekeleza baadhi ya makubaliano yaliyokuwepo baina yake na uongozi wa klabu hiyo.

Kwa mujibu wa kocha huyo amesema: "Ni Kweli nimesimama kufanya kazi katika klabu ya TOTO na inatokana na kutotekelezwa kwa baadhi ya mambo na viongozi wa wa timu"

Kocha Almasi Moshi amesema mambo ambayo yameshindwa kutekelezwa ni ya  Kiufundi,Wachezaji pamoja na mwalimu (YEYE) , Amesema hawezi kufundisha timu wakati wachezaji wanamalalamiko ya Mishahara, Hawapati chakula na Mambo mengine.

No comments: