Tetesi Za Usajili Manchester united, Atletico Madrid, Chelsea..

nintchdbpict000325949637
Manchester United huenda wakamsajili Antoine Griezmann mwezi Januari kama klabu yake itafanikiwa kumrejesha nyumbani Diego Costa.

Klabu ya Chelsea inataka kumfanya Eden Hazard kuwa mchezaji anayelipwa zaidi kwenye mkataba mpya anaotarajia kuusaini,atakaokuwa akilipwa pauni 300,000 kwa wiki ikiwa ni njia ya kumfanya asiifikirie Real Madrid.

Manchester United wameonesha nia ya kumhitaji Klapin Diatta ambaye siku zote amekuwa akiihitaji klabu hiyo kama ndoto yake.

Chelsea wapo mbioni kumsajili nyota wa PSG Edson Cavani mnamo mwezi Januari endapo nyota huyo atakubali kujiunga nao.

T0ttenham na West Ham wapo kwenye vita kali ya kuiwania saini ya kinda mwenye umri wa miaka 17 Mitch Candlin ambaye itakuwa ni kwa mara ya kwanza kwake kusaini mkataba wa kucheza daraja la juu.


Rio Ferdnand amesema kwamba Fillipe Coutinho bado hajakomaa kuchezea klabu ya Barcelona.

No comments: